Usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Mali, Lassine Kouma (21), anayekipiga katika klabu ya Stade Malien ni kama umehitimisha hesabu za Yanga upande wa nyota wa kigeni
Inaelezwa mlinda lango Djigui Diarra ndiye aliyehakikisha Kouma anatua Yanga baada ya nahodha huyo wa Stade Malien kuwasiliana nae akiomba apewe uzoefu kuhusu ligi ya Tanzania na klabu ya Simba iliyokuwa inakaribia kumsajili
Diarra 'akafanya umafia' kwa kuwasiliana na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said juu ya kiungo huyo ambaye pia alikuwa kwenye rada za Al Hilal na kumshawishi ajiunge na Yanga
Usajili wa Lassime utakamilisha idadi ya nyota watano wa kigeni waliosajiliwa na Yanga katika dirisha hili
Nyota wengine ni Moussa Balla Conte, Celestine Ecua, Mohammed Doumbia na Andy Boyeli
Nyota watano ambao wamepisha sajili hizo ni Kennedy Musonda, Clatous Chama, Stephane Aziz Ki, Khalid Aucho na Jonathan Ikangalombo ambaye inaelezwa uongozi uko katika mazungumzo ya kumalizana nae