Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua atacheza timu moja tu Tanzania ambayo Yanga Sc
Katika dirisha hili la usajili kumekuwa na tetesi nyingi kumuhusu MVP huyo mtarajiwa wa ligi kuu ya NBC juu ya hatma yake na Yanga
Wapo wanaodai kuwa Pacome hajaongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai Pacome tayari amesaini upande wa pili wa watani, klabu ya Simba
Kamwe amesema anachofahamu yeye Pacome atacheza Yanga tu hapa Tanzania lakini timu nyingine ambazo zinatamani kuwa nae, zinaweza kutumia mbinu mbadala
"Ukisikia Pacome anahusishwa na tetesi za timu nyingine maana yake ni mchezaji mzuri. Ila kwa sasa watu wote ambao wanamuhitaji Pacome, kitu pekee ambacho tunaweza kuwasaidia ni kopo a blichi"
"Watafute mchezaji wao yeyote wampake blichi afanane na Pacome lakini Zouazoua mwenyewe sioni kama kuna timu atacheza Tanzania zaidi ya Yanga Sc"
"Kwa yeyote anayetamani kitu kingine cha Pacome basi namba zangu zipo njoo hata DM oda kopo la blichi la Pacome unaweza kwenda kuwapaka wachezaji wako na ukafurahia zile blichi na kuhisi kama umeshampata Pacome," alitamba Kamwe
Inaelezwa klabu ya Yanga ilimuongeza mkataba Pacome mapema kabla hajarejea kwao Ivory Coast kwa mapumziko baada ya msimu kumalizika
Pacome, Dickson Job, Maxi Nzengeli na Duke Abuya wote wameongeza mikataba kuendelea kuitumikia Yanga