Yanga kwenda kamili Nairobi kushiriki mshindano ya SportPesa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2018
Yanga kwenda kamili Nairobi kushiriki mshindano ya SportPesa
Yanga ni miongoni mwa timu nne kutoka Tanzania zitakazoshiriki mashindano ya Sportpesa Super Cup ambayo mwaka huu yanafanyika nchini Kenya.

Mashindano hayo yataanza Juni 03 mpaka Juni 10 2018 yakifanyika kwenye dimba la Kasarani, Nairobi Kenya.

Timu nyingine kutoka Tanzania zitakazoshiriki mashindano hayo ni Simba, Singida United na JKU.

Nyingine nne zitatoka nchini Kenya ambazo ni Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

Timu zitakazoingia robo fainali kwenye mashindano hayo zitapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola 7,500 na 10,000 kila mmoja.

Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park nchini Uingereza.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba amesema timu bingwa itapata faida zaidi ya kucheza na Everton.

Tarimba amesema nchini Uingereza timu hiyo itaenda kujifunza uendeshaji wa mpira, Nidhamu ya wachezaji na matunzo ya viwanja vya soka.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema timu hiyo itashiriki kikamilifu mashindano ya mwaka huu.

Yanga inayoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi ikiwa kundi moja na Gor Mahia, itaweza kutumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Gor Mahia mwezi Julai.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’