Folz kulisuka upya benchi lake la ufundi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2025
Folz kulisuka upya benchi lake la ufundi

Yanga imebakiza hatua chache kumalizia usajili, lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Romain Folz kuna mabadiliko anayoyafanya akipanga kushusha watu wengine wawili wapya katika benchi la ufundi.

Kocha huyo kijana mwenye umri wa miaka 35, aliyetambulishwa wiki iliyopita tayari ameshashusha watu wawili mapema, lakini bado kazi hiyo ataendelea nayo ikidaiwa kwa sasa amepata ruhusa ya kuongeza watu wengine wawili ili mambo yawe mepesi kwa msimu wa kwanza akiwa na kikosi hicho.

Awali Folz alikubaliana na maombi ya mabosi wa Yanga juu ya kuwabakisha wasaidizi aliowakuta katika benchi la ufundi lililoachwa na mtangulizi wake, Miloud Hamdi, lakini kuna mambo yamebadilika.

Kuna watu watatu katika benchi la Yanga wanaondoka wa kwanza ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Abdihalim Moallin, mtaalamu wa uchambuzi wa mikanda ya video (video analyst), Mpho Maruping na daktari wa viungo Sekhwela Seroto.

Watatu hao wote wanatajwa kuelekea Algeria kuungana na Sead Ramovic katika klabu ya CR Belouzdad, hatua ambayo itamlazimisha Folz kuunda upya benchi hilo kabla ya kwenda katika kambi ya maandalizi ya msimu.

Hadi sasa katika benchi hilo la Yanga, amesalia kocha wa makipa mzawa Soud Slim na kocha wa mazoezi ya viungo Taibi Lagrouni raia wa Morocco.

Ukiacha kocha msaidizi, Folz atamleta mtaalam wa uchambuzi wa mikanda atakayeungana na Paul Mathew ambaye ameshafika nchini, akija kuchukua nafasi ya Mkurugenzi wa ufundi. Folz pia anatajwa kumleta kocha mpya wa makipa Majdi Mnasria, raia wa Tunisia.

Nafasi ya daktari wa viungo, Yanga imeshaanza harakati za kumrudisha Mtunisia Youssef Ammar ambaye alkuwa nafasi hiyo kabla ya kuondoka alipokuja Miguel Gamondi.

Folz anataka wasaidizi hao waje mapema kabla ya timu hiyo kuondoka nchini Agosti 13 kwenda Rwanda kwa mualiko maalum na wenyeji wao Rayon Sport watakaocheza nao mchezo wa kirafiki Agosti 15.

Baada ya mchezo huo, Yanga huenda ikaelekea Misri kuendelea na maandalizi ya msimu mpya

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’