Yanga tayari kuanza pre-season 2025/26

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Aug 2025
Yanga tayari kuanza pre-season 2025/26

Likizo imemalizika! Ndivyo unavyoweza kusema kwani leo kikosi cha Yanga chini ya Kocha Mkuu Romain Folz kinatarajiwa kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025-26

Juzi na jana Yanga iliendesha zoezi la kuwafanyia wachezaji vipimo vya afya ambapo kulingana na ratiba iliyotolewa siku chache zilizopita, Folz ameagiza kuanza maandalizi leo ili kukiandaa kikosi chake kwa wiki mbili kabla ya kuelekea Rwanda kuikabili Rayon Sports katika kilele cha Rayon Day August 15

Yanga inatarajiwa kufanya maandalizi yake katika uwanja wa KMC Complex. Maandalizi hayo yatajumuisha wachezaji wote ambao hawako katika majukumu ya timu za Taifa

Nyota wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha hili nao wako jijini Dar es salaam Yanga ikiwa bado inaendelea kuwatambulisha wengine

Jana Yanga ilimtambulisha mshambuliaji Andy Boyeli ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuendelea leo. Nyota wengine wa kigeni wanaosubiri utambulisho ni kiungo fundi Mohamed Doumbia na kiungo mshambuliaji Ecua Celestine

Wachezaji hao tayari wako jijini Dar es salaam wakiungana na Moussa Balla Conte, Lassine Kouma na Boyeli ambao tayari wametambulishwa

Beki wa kushoto Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' nae anasubiri utambulisho, hata hivyo yeye yuko kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayoshiriki michuano ya CHAN

Nyota wengine wa Yanga ambao wako kwenye kikosi cha Stars kwa ajili ya CHAN ni Dickson Job, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya, Shekhan Khamis na Clement Mzize

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’