Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) linajiandaa kufanya droo ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2025-2026.
Tukio hilo litafanyika katika mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa tovuti ya Qatari ya WinWin, hafla hiyo imepangwa kufanyika Agosti 09 saa 8 mchana kwa saa za Tanzania.
Yanga itaiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa sambamba na watani zao Simba, huku Azam FC na Singida Black Stars wakiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.
Ratiba ya awali ya mashindano ya Afrika (msimu wa 2025/2026)
- Raundi ya kwanza ya awali: Septemba 19 hadi 28, 2025 (mechi za nyumbani na ugenini)
- Raundi ya pili ya awali: Oktoba 17 hadi 26, 2025
- Hatua ya makundi: Novemba 2025 hadi Februari 2026
- Robo fainali: Machi 2026
- Nusu fainali: Aprili 2026
- Fainali: kati ya Mei 8 na Mei 24, 2026
ADVERTISE HERE