Mudathir anaendelea kung'ara CHAN 2024

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Aug 2025
Mudathir anaendelea kung'ara CHAN 2024

Kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mudathir Yahya anaendelea kung'ara katika michuano ya CHAN 2024 inayoendelea jijini Dar es salaam jana akiiongoza Stars kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mauritania kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mudathir alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ambao ulishuhudia dakika 90 za aina yake Stars ikifunga bao la ushindi dakika za lala salama kupitia kwa Shomari Kapombe

Kiungo huyo wa mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga, amekuwa nguzo ya safu ya kiungo ya kikosi cha Dtars akishirikiana vyema na viungo wenzake Feisal Salum 'Fei Toto' na Yusuph Kagoma ambaye hata hivyo jana alicheza kwa dakika 45 tu baada ya kupata kadi ya njano mapema ambapo kadri mchezo ulivyoendelea kulikuwa na hatari ya kupewa kadi ya pili ya njano

Mudathir ameendeleza ubora alioonyesha kwenye michuano hiyo tangu mchezo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso

Stars inaongoza kundi B ikifikisha alama 6 baada ya ushindi dhidi ya Mauritania ikijiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya mtoano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’