Vigogo wanapigana vikumbo Jangwani kumpata Mzize

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2025
Vigogo wanapigana vikumbo Jangwani kumpata Mzize

Unaweza kusema mshambuliaji Clement Mzize ndio habari ya mjini kwa sasa katika soka la Tanzania akiendelea kuwagonganisha vigogo pale Makao Makuu ya Yanga, Jangwani wakiwania saini yake

Mpaka sasa tayari Yanga ina makubaliano na klabu ya Al-Sadd SC ya Qatar lakini klabu hiyo bado haijafikia makubaliano na Mzize mwenyewe juu ya maslahi yake hasa upande wa mshahara

Juzi klabu ya Al Masry nayo ikajitosa ikituma ofa inayokadiriwa kufikia Tsh Bilioni 1.5 ambayo hata hivyo ilikataliwa na Yanga kwani tayari Al-Sadd SC wameweka mezani Tsh Bilioni 2.2

Klabu ya Esperance ya Tunisia nayo inatarajiwa kutuma ofa ndani ya siku chache zijazo kujaribu kumshawishi Mzize kuelekea Tunisia

Al Ittihad ya Libya na Zamalek nazo zilituma ofa ambazo hata hivyo hazikumshawishi mchezaji huyo upande wa maslahi

Uongozi wa Yanga umefungua milango kwa Mzize kwenda kutafuta changamoto nje ya mipaka ya Tanzania, lakini inaelezwa kinachofanya mpaka sasa yuko nchini ni upande wa wasimamizi wake

Zamalek walikuwa katika hatua za mwisho kumsajili lakini walisitisha mpango huo wakidai gharama ziliongezeka katikati ya mchakato kinyume na makubaliano ya awali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’