Kiungo wa zamani wa Yanga Haruna Niyonzima leo alijumuika katika mazoezi ya mwisho ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Amahoro huko Rwanda
Historia yake na klabu ya Yanga inamfanya Niyonzima awe legendari na balozi wa kudumu wa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara
Kabla ya kujumuika mazoezini, Niyonzima alitambulishwa kisha kusalimiana na wachezaji pamoja na nchi la ufundi
Ama kwa hakika lilikuwa tukio la kipekee kumshuhudia Niyonzima kwa mara nyingine katika uzi wa Yanga





ADVERTISE HERE