FT : Rayon Sports 1-3 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Aug 2025
FT : Rayon Sports 1-3 Yanga

Yanga imebeba taji jingine mapema baada ya kuichapa Rayon Sports mabao 3-1 katika mchezo wa kilele cha Rayon Sports Day uliopigwa uwanja wa Amahoro, Rwanda

Bao la mapema la kujifunga Aziz Andabwile lilikaribia kuvuruga mipango ya Yanga katika mchezo huo lakini kikosi cha kocha Romain Folz kilionyesha ukomavu wake

Mshambuliaji Andy Boyeli aliisawazishia Yanga akiitendea haki pasi ya Pacome Zouzoua kabla ya kumtengenezea Pacome kufunga bao la pili na kuipeleka Yanga mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao 2-1

Katika kipindi cha kwanza Yanga ilitengeneza nafasi za wazi mbili au tatu lakini unaweza kusema mwamuzi alijitahidi kupunguza machungu kwa wenyeji

Kipindi cha pili Folz alifanya mabadiliko karibu timu nzima, nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto akifunga bao la tatu dakika za lala salama

Katika mchezo huo, Yanga ilimtambulisha winga Edmund John ambaye amesajiliwa kutoka klabu ya Singida BS

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
42m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’