Chikola ashukuru sapoti ya mashabiki wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2025
Chikola ashukuru sapoti ya mashabiki wa Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Offen Chikola, ameonyesha furaha na shukrani kubwa kwa sapoti anayopata kutoka kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo, akiahidi kuendelea kupambana kwa ajili ya heshima ya nembo ya Yanga na kuhakikisha timu inafikia malengo yake.

Chikola, ambaye ni miongoni mwa sajili za ndani zilizopata mapokezi makubwa, amesema moyo na shauku ya mashabiki kumwamini kumempa nguvu zaidi ya kuonyesha uwezo wake uwanjani.

Juzi, kocha mkuu wa Yanga, Romain Folz, alimpa dakika 45 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports uliochezwa kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali. Katika muda huo, Chikola alionyesha kiwango kizuri kilichowafurahisha mashabiki waliokuwepo uwanjani pamoja na wale waliokuwa wakifuatilia kutoka nyumbani.

"Mimi najivunia na naheshimu mchango wa mashabiki wa Yanga. Kikubwa waendelee kuisapoti timu yao kwani sisi wachezaji tunawategemea sana wao. Wingi wao uwanjani unatupa hamasa kubwa bila kujali tunacheza nyumbani au ugenini," alisema Chikola.

Aidha, winga huyo alifafanua kuwa amekuwa akipata msaada mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzake, jambo linalomsaidia kuimarisha kiwango chake kila siku.

"Nimekuwa pia nikizungumza na wachezaji wenzangu ambapo wapo wanaonipongeza ninapofanya vizuri na kunishauri nini napaswa kufanya zaidi ili kuinufaisha timu. Naheshimu mchango wa kila mmoja kwani sote lengo letu ni moja, kuhakikisha Yanga inafanya vizuri na kufikia malengo yake," aliongeza.

Chikola ametua Yanga katika dirisha hili la usajili akitokea klabu ya Tabora United. Mwanzo wake mzuri ndani ya mabingwa hao wa nchi ni dalili kuwa huenda akawa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’