Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika michuano ya CHAN 2024, Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amewapa mapumziko ya siku chache nyota wa Yanga waliokuwa katika kikosi cha Stars
Mabeki Dickson Job, Ibrahim Bacca na Mohammed Hussein, viungo Mudathir Yahya, Shekhan Khamis na mshambuliaji Clement Mzize walikuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kilitolewa hatua ya robo fainali baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Morocco
Wachezaji hao wanatarajiwa kujiunga na wenzao mwanzoni mwa Septemba au baada ya mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Niger ambao utapigwa Septemba 09
Kuna uwezekano mkubwa wote watajumuishwa katika kikosi hicho ambacho kitajumuisha wachezaji wanaocheza ndani na nje ya nchi
Inaelezwa Folz ametoa siku za mapumziko ambapo kwa wale ambao hawatajumuishwa kikosi cha Stars, watahitaji kuripoti kambini Avic Town kuendelea na maandalizi ya wiki ya Mwananchi na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaopigwa Septemba 16