Tutaendeleza tulipoishia msimu uliopita - Gumbo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2025
Tutaendeleza tulipoishia msimu uliopita - Gumbo

Baada ya Bodi ya Ligi (TPLB) kutangaza ratiba ya ligi kuu 2025/26 hapo jana, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga Rodgers Gumbo amesema Yanga itaingia msimu huu kuendeleza mafanikio yao ya msimu uliopita

Mabingwa hao watetezi, msimu uliopita walitwaa mataji yote ya ndani wakijihakikishia taji la ligi kuu katika mchezo wa mwisho wa msimu dhidi ya watani zao Simba kwa ushindi wa mabao 2-0

Gumbo ametamba kwa maboresho makubwa ya kikosi yaliyofanyika pamoja na maboresho ya kambi yao Avic Town, haoni sababu ya Yanga kushindwa kuendeleza ubabe

“Tumeiona ratiba hatuna shida nayo sana, ninachosema, Yanga tupo tayari kwa msimu huu mpya ambao tutauanza kuanzia mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya watani wetu Simba"

“Baada ya msimu uliopita kumalizika, Uongozi wetu ulikaa chini na kufanya tathimini kubwa ya kikosi chetu, pia hata kuangalia wapinzani wetu lakini kikubwa tumetengeneza timu kubwa. Malengo yetu ni makubwa ilitulazimu usajili wetu uwe wa viwango vya mbali, ndiyo maana unaona tulisajili timu itakayocheza kwa nguvu mashindano ya Afrika.

“Unajua kama utakuwa na timu kubwa ya kushindana kibabe katika mashindano ya Afrika maana yake hata hapa ndani una nafasi kubwa ya kufanya makubwa,” Gumbo alinukuliwa na Mwanaspoti

Aidha Gumbo alisema uongozi wa klabu hiyo baada ya kuiboresha kambi yao ya Avic Town, pia kutakuwa na maboresho makubwa ya masilahi kwenye kuongeza ushindani ndani ya kikosi chao na hata kwenye mashindano kijumla.

“Tuliwaleta wataalam wameiboresha kambi yetu na sasa imekuwa ya kisasa, pale ndipo ambapo panatupa jeuri ya kujiandaa tunapotaka kwenda kukutana na timu yoyote"

“Ukiacha hilo idara yetu ya mashindano, tumepitia yale tuliyoyafanikisha msimu uliopita, kutakuwa na maboresho makubwa ili kuhakikisha wachezaji wetu wanajituma kuitafutia ushindi klabu yetu"

Yanga itaanza msimu 2025/26 nyumbani Septemba 24, 2025 kwa kuvaana na Pamba Jiji kabla ya kuifuata ugenini Mbeya City iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, siku ya Septemba 30, siku chache baada ya kumalizana na Wiliete Banguela ya Angola katika mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi ya awali baina yao itapigwa Septemba 19-21.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’