Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika (ACA), Injinia Hersi Ally Said jana alishiriki kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji cha CAF kilichofanyika Nairobi, nchini Kenya.
Hersi pia alipata nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu maendeleo ya Vilabu Barani Afrika na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani, Gianni Infantino pamoja na Rais wa CAF, Patrice Motsepe.
Baadae, Hersi na viongozi wengine wakubwa wa mpira Barani Afrika, walipata fursa ya kushuhudia mchezo wa Fainali ya Kombe la CHAN, Kati ya Morocco na Madagascar.
Mchezo huo ulipigwa dimba la Kasarani Morocco wakiibuka mabingwa kwa kuifunga Madagascar mabao 3-2



ADVERTISE HERE