Mwamnyeto awaalika mashabiki wiki ya Mwananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2025
Mwamnyeto awaalika mashabiki wiki ya Mwananchi

Klabu ya Yanga itahitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi mnamo Septemba 12 kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Bandari FC ya Kenya.

Tamasha hilo, ambalo limekuwa utamaduni mkubwa wa Wananchi, linalenga kuwatambulisha mashabiki wachezaji wapya pamoja na wale wa kikosi cha zamani pamoja na kukaribisha msimu mpya.

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, ametoa mwaliko maalum kwa mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kushuhudia kile ambacho klabu imewaandalia.

Mwamnyeto amesema maandalizi yanaendelea vyema Avic Town akiwahakikishia mashabiki wameandaliwa burudani ya aina yake kutoka kwa timu yao

“Sisi tunaendelea vyema na maandalizi ya siku hii kubwa na yenye furaha kwa klabu ya Yanga. Niwaambie mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia kile tulichowaandalia. Kila mchezaji hapa kambini ana shauku kubwa ya kusubiri siku hii ya aina yake,” alisema Mwamnyeto.

Yanga, ikiwa kambini Avic Town, inaendelea na maandalizi yake kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kuelekea tamasha hilo kubwa ambalo limekuwa tukio muhimu kwenye kalenda ya mabingwa hao wa nchi.

Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia burudani ya kipekee uwanjani, ikiwemo kutambulishwa kwa kikosi kipya, burudani, na mchezo wa kirafiki dhidi ya wageni kutoka Kenya, Bandari Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’