Kesho Jumapili Septemba 07 2025, klabu ya Yanga itafanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama ambao unafanyika kwa mujibu wa katiba ya klabu
Takribani matawi 160 nchi nzima yatashiriki Mkutano huo baada ya kukidhi vigezo lakini pia mwaka huu kuna matawi kutoka nje ya nchi yatashiriki
Matawi 6 kutoka nje ya Tanzania yatashiriki Mkutano huo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu ya Yanga
Matawi hayo yapo katika nchi za Kenya, DR Congo, Afrika Kusini, Marekani, China na Japan
Matawi haya kila moja lina Wanachama zaidi ya 100 na hivyo kuwa vigezo vya kushiriki Mkutano Mkuu utakaofanyika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE