Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amefichua kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Romain Folz aliomba mshambuliaji Clement Mzize asiondoke klabuni katika dirisha hili kwa kuwa anamuhitaji katika kikosi chake
"Tulipokea ofa nyingi kwa ajili ya mshambuliaji Clement Mzize. Niwaambie tu ofa ya mwisho tuliyopokea ni Dola Milioni 2 (Bil 5) lakini tukakataa kwa sababu sisi sio Akademi"
"Hatuwezi kumuuza Mzize kwa gharama yoyote kwa sababu tunamuhtaji msimu ujao. Kocha Romain Folz aliniambia anamuhitaji Mzize kwa ajili ya mipango yake msimu huu"
"Tulichofanya ni kuboresha maslahi ya mchezaji ambapo kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi ndani ya kikosi cha Yanga," alisema Hersi
Hersi amesema Yanga imedhamiria kushindana msimu ujao hasa katika michuano ya ligi ya mabingwa hivyo hawawezi kuwauza wachezaji wao muhimu
Mzize ataendelea kutumikia mkataba wake wa miaka miwili uliobaki ndani ya Yanga