Tutaandika historia wiki ya Mwananchi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2025
Tutaandika historia wiki ya Mwananchi - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa tayari kwa Tamasha kubwa la burudani, kilele cha wiki ya Wananchi ambalo litafanyika kesho Ijumaa katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kamwe amesema jukumu la kwanza la mashabiki ni kununua tiketi kwa wingi ili kujaza dimba la Mkapa. Lakini pia wanapaswa kuongeza ubora wa tamasha kwa kuhakikisha wanaibua shangwe majukwaani

Kamwe amesema maandalizi ya uwanja wa Benjamin Mkapa yalianza jana muda mfupi baada ya kumalizika kwa Tamasha la Simba

"Maandaizi yetu yalianza mara moja baada ya kumalizika kwa tamasha la wenzetu. Nafikiri hadi kufikia jioni wakati Bandari Fc watakapokwenda uwanjani kufanya mazoezi ya mwishoni maandalizi yote yatakuwa yamekamilika"

"Tamasha hili tumeligawanya katika maeneo manne, eneo la kwanza linamilikiwa na mashabiki wa Yanga. Hili ni eneo la kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa na kuwa na shangwe"

"Hatuwezi kwenda kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi halafu tukawa tumepooza. Niwaombe mashabaki na wanachama tutengeneze nguvu ya kutosha kwa ajili ya siku ya kesho"

"Eneo la pili ni burudani, tumefanya kikao na wasanii wote ambao watatoa burudani kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya kesho"

"Miongoni mwa wasanii tutakaokuwa nao ni Meja Kunta, Dula Makabila, Mzee wa Bwax, D-Voice, Dogo Pateni hawa wote ni wakali wa singeli. Zuchu ndiye atakayehitimisha shoo za wasanii, ametuandalia burudani ya aina yake"

"Eneo la tatu ni eneo la mpira, tutakuwa na mechi tatu. Yanga Princess watacheza dhidi ya Mashujaa Queens. Kutakuwa na mechi kati ya Staff wa Yanga dhidi ya wasanii mashabiki wa Yanga. Mechi ya tatu ni Yanga dhidi ya Bandari Fc. Sisi tunatambua thamani ya mashabiki wetu ambao wametoka kila kona ndani na nje ya nchi. Hivyo mtarajie kuwaona wachezaji wote dimbani kuanzia Celestin Equa, Mussa Balla Conte na wengine wote"

"Niwahakikishie mtaiona Yanga ileile sisi hatuogopi mtu, tutashusha kikosi chetu kamili na tutacheza katika daraja letu na uchu uleule ili tukate kiu ya burudani kwa mashabiki wetu," alitamba Kamwe

Kamwe pia alibainisha kuwa eneo la nne ni la viongozi wa Yanga ambapo wamewaandalia zawadi maalum wanachama na mashabiki wa Yanga

"Nimeambiwa kwenye ratiba, viongozi wa Yanga wako na zawadi kubwa ya kuwapa mashabiki na wanachama wetu Benjamin Mkapa Stadium. Ni zawadi gani sijaambiwa, ni tukio gani mimi sijui. Kwa aina ya maandalizi bila shaka ni tukio kubwa hivyo niwaombe mashabiki wa Yanga tuje kwa wingi uwanjani tupate zawadi hiyo," aliongeza Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’