Kwa busta hili la Yanga, vilio vitaendelea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2025
Kwa busta hili la Yanga, vilio vitaendelea

Tamasha la Wiki ya Mwananchi limehitimishwa kwa kishindo jana pale Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Yanga SC iliwapa mashabiki wao burudani na matumaini makubwa kwa msimu mpya.

Bao la dakika ya pili kutoka kwa Celestin Equa lilitosha kuipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bandari FC ya Kenya, katika mchezo wa kirafiki uliofungia tamasha hilo. Lakini kwa mashabiki wa Wananchi, habari kubwa haikuwa ushindi pekee, bali namna kikosi kipya kilivyoonyesha kiwango cha juu na ari ya kupigania nembo ya klabu hiyo kubwa nchini.

Mashabiki walishuhudia jinsi kila mchezaji aliyepewa nafasi alivyojituma, huku nyota wapya wakionekana kuendana na falsafa ya klabu kwa haraka. Jukwaani, shangwe zilithibitisha kuwa matumaini kwa kikosi hiki yameongezeka mara dufu.

Pengine changamoto kubwa sasa inabaki kwa Kocha Romail Folz. Ndani ya kikosi chake ana hazina ya wachezaji bora 26, lakini kwenye kila mchezo anahitaji kuwatumia 11 pekee. Ushindani wa nafasi ni mkubwa, na hilo linaonyesha namna Yanga ilivyojipanga kila idara kwa ajili ya msimu mrefu unaokuja.

Jana, Folz alitumia mchezo huo kutoa nafasi kwa wachezaji wengi, jambo lililowapa mashabiki ladha ya kikosi kipana na chenye ubora. Haitashangaza kama watani zao wa jadi, Simba, walikuwa wakifuatilia mchezo huu kwa makini na bila shaka baadhi yao walivurugwa kuona Yanga ikicheza kwa nidhamu ya juu ya kimbinu na utimamu wa mwili.

Ikumbukwe, huu ulikuwa mchezo wa pili wa Yanga kuonekana mubashara baada ya ule wa Rayon Sports Day nchini Rwanda. Tofauti kubwa sasa ni kwamba Yanga imeonekana kuimarika zaidi, wachezaji wakiwa “fit” na mbinu zikionekana kuiva.

Wiki ya Mwananchi mwaka huu imetoa ujumbe mmoja mzito, vilio kwa wapinzani vitaendelea msimu huu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’