CAF yabadili uwanja, Wiliete vs Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2025
CAF yabadili uwanja, Wiliete vs Yanga

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limebadilisha uwanja wa mchezo wa mkondo wa kwanza hatua  ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Wiliete Banguela dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 19

Awali, Yanga ilitarajiwa kuanza kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa kwa kucheza ugenini dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola mjini Benguela Septemba 19, kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, CAF imeuhamishia mchezo huo jijini Luanda, mji mkuu wa Angola

Hatua hiyo ni ahueni kwa Yanga kwani wangelazimika kusafiri kwa zaidi ya saa nane kwa gari kutoka Luanda kwenda Benguela, au kutumia angalau saa moja kwa ndege.

“Tumepata unafuu mkubwa. Sasa mchezo utafanyika mjini Luanda tofauti na awali ambapo tulipaswa kutafuta tena njia ya kufika Benguela. Hii ni faida kwetu,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa ratiba, mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Septemba 19, saa 12 jioni na mechi ya marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 27, saa 10 jioni

Kabla ya mchezo huo, Yanga inakabiliwa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Simba ambayo itapigwa kesho Jumanne, Septemba 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’