Yanga kuendeleza ubabe wake kwa Simba leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2025
Yanga kuendeleza ubabe wake kwa Simba leo?

Leo Jumanne, Septemba 16, 2025, macho ya mashabiki wa soka nchini yatakuwa yameelekezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ambapo Yanga SC na Simba SC watakutana katika pambano la Ngao ya Jamii kuanzia saa 11 jioni.

Ni dabi ya Kariakoo nyingine yenye msisimko wa kipekee, ikiwakutanisha wapinzani wa jadi wa muda mrefu.

Kwa upande wa Yanga SC, hii ni mechi inayokuja kwa wakati sahihi. Wanajangwani wanabeba rekodi ya kuvutia baada ya kushinda mechi tano mfululizo dhidi ya Simba katika mashindano yote, hali inayowapa kujiamini zaidi kuelekea mtanange wa leo.

Mashabiki wa Yanga wanatambua kuwa ushindi wa leo si tu wa kuongeza taji jingine kabatini, bali pia ni ishara ya kuendeleza ubabe wao wa miaka ya karibuni mbele ya mahasimu wao.

Kocha mpya wa Yanga, Romain Folz, raia wa Ufaransa, anatarajiwa kuiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza katika dabi ya Kariakoo. Folz ameanza kazi yake kwa kishindo, akiipeleka Yanga kwenye pre-season isiyo na doa baada ya kushinda mechi zote za kirafiki walizocheza.

Matokeo hayo yamewajengea wachezaji morali na kuonesha kuwa falsafa ya kocha huyo imeanza kukolea kikosini.

Wakati Simba wakihaha kurejesha heshima baada ya kupoteza mechi tano mfululizo dhidi ya Yanga, Wanajangwani wanaingia wakiwa na confidence ya hali ya juu. Kikosi chao kimejaa wachezaji wenye uzoefu wa mechi kubwa pamoja na nyota wapya walioongeza ubora na ushindani ndani ya timu.

Kwa mtazamo wa wengi, mazingira yote yanaipa Yanga nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu. Rekodi nzuri dhidi ya Simba, morali ya wachezaji, pamoja na mbinu mpya za kocha Folz, vinaifanya Yanga kuwa timu yenye nguvu zaidi kuelekea pambano la leo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’