Yanga yatua Angola na matumaini kibao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2025
Yanga yatua Angola na matumaini kibao

Mtendaji wa klabu ya Yanga Andre Mtine amesema wametua Angola wakiwa na dhamira moja tu, kushinda mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete Sc utakaopigwa kesho Ijumaa

Kikosi cha Yanga kilitua Luanda jana kuelekea mchezo huo utakaopigwa ndani ya jiji la Luanda majira ya saa 12 jioni kwa saa za Tanzania

Mtine ambaye ameongoza msafara wa Yanga, amesema wanatambua wanakwenda kucheza na timu imara hivyo benchi la ufundi limefanya maandalizi ya kina ili kuhakikisha wanaanza vyema katika michuano hiyo

"Tumewasili hapa Angola salama kuelekea mchezo wetu wa ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete Sc. Tumefanya maandalizi ya kutosha, benchi letu la ufundi limepata nafasi ya kuwasoma wapinzani wetu na kufanya maandalizi sahihi kuelekea mchezo huu"

"Niwaombe mashabiki watuombee dua ili tuweze kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na kuhakikisha tunatimiza malengo yetu," alisema Mtine

Naye Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema baada ya kutua Angola jana, usiku timu ilifanya mazoezi maalum ya Gym kuondoa uchovu na leo watafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja utakaotumika hapo kesho

Yanga iliondoka Tanzania alfajiri ya jana takribani masaa nane baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0

Ni kama Wiliete Sc wamechagua mchezo huo kupigwa Septemba 19 wakiamini pengine nyota wa Yanga bado watakuwa na uchovu wa dabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’