Matchday; Wiliete vs Yanga, CAF CL, PR1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2025
Matchday; Wiliete vs Yanga, CAF CL, PR1

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Young Africans (Yanga SC), leo wanaanza safari yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26 kwa kuvaana na Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Novemba 11, Luanda, majira ya saa 12 jioni kwa saa za Tanzania.

Kikosi cha Yanga kilitua Luanda Jumatano jioni, na jana Alhamisi kilifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja utakaotumika kwa mchezo huo, kuhakikisha maandalizi yamekamilika kabla ya mtihani wa leo.

Kwa upande mmoja, hii ni mechi ya timu yenye historia na uzoefu mkubwa barani Afrika dhidi ya timu changa inayojaribu kutengeneza alama yake. Yanga, mara kadhaa ikitinga hatua ya makundi ya CAFCL, imeweka malengo makubwa msimu huu: kuhakikisha inavuka hatua ya awali na mtoano ili kufanikisha safari ya kufika makundi.

Kwa upande mwingine, Wiliete SC ni timu changa yenye takribani miaka minane tangu ianzishwe, lakini imepiga hatua kubwa ndani ya muda mfupi. Kupata nafasi ya kumaliza ligi kuu ya Angola katika nafasi ya pili msimu uliopita na kufuzu michuano ya CAF kwa mara ya kwanza ni ishara ya ukuaji wa kasi na malengo makubwa waliyojiwekea.

Kocha Mkuu wa Yanga, Romain Folz, amesema kuwa wachezaji wake wako tayari kupambana na kuhakikisha wanapata matokeo chanya ugenini:

Kwa Yanga, ushindi leo utakuwa nguzo muhimu katika malengo yao ya kufuzu hatua inayofuata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’