Mshamuliaji wa Yanga Clement Mzize huenda akaukosa mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu huu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mzize alipata majeraha katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete Sc ambao ulipigwa Septemba 19 huko Angola
Wakati Mzize akikosekana, habari njema kwa Wananchi ni kurejea kwa mshambuliaji Andy Boyeli ambaye alikuwa majeruhi

Boyeli aliumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Tabora United wakati Yanga ikiwa kwenye pre-season
Boyeli alishiriki kikamilifu mazoezi ya Yanga jana yakiwa ni maandalizi ya kuikabili Pamba Jiji
Yanga imepania kuanza vyema msimu 2025/26 kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Pamba Jiji ili kuzindua rasmi safari ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo