Kila mchezaji ana umuhimu kikosini - Folz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Sep 2025
Kila mchezaji ana umuhimu kikosini - Folz

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema anajivunia kuwa na kikosi kipana kilichosheheni wachezaji ambao wako tayari kutumika katika kila mchezo

Folz amesema kila mchezaji katika kikosi chake ni muhimu lakini anapaswa kutumia wachezaji 11 wa kuanza katika kila mechi hivyo haimaanishi kama mchezaji hajaonekana katika mechi moja sio muhimu

Kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Folz amesema kuwa wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na dhamira ya kuanza vyema msimu kwa kuibuka na ushindi

"Tunakwenda kucheza mchezo wa tatu wa ushindani, kwetu ni mchezo muhimu sana na tumejianda kufanya vizuri. Tupo tayari kwenye kila idara. Tumepata Pre-Season bora ambayo itatusaidia sana msimue"

"Msimu huu kila mechi tunahitaji kupata alama tatu kila mechi. Yanga ni timu kubwa, malengo yetu ni kutwaa ubingwa wa ligi. Tunawachezaji bora sana na kikosi kipana. Kila Mchezaji kwangu ni muhimu. Unaweza kumuona mchezaji mmoja leo, mchezo unaokuja usimuone. Nitatoa nafasi kwa kila mchezaji kulingana na anavyojituma"

"Tutarajie kuona mabadiliko ya wachezaji katika mechi zetu lakini muhimu ifahamike tuna timu imara yenye wachezaji ambao wako tayari kuipigania timu hii ili tufanye vyema na kutimiza malengo yetu," alisema Folz

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake,  beki Frank Assink alisema mashabiki wanajua Yanga ni timu nzuri na kesho watarajie kuona kiwango kizuri kutoka kwa timu yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’