FT : Yanga 2-0 Wiliete, CAFCL PR2

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Sep 2025
FT : Yanga 2-0 Wiliete, CAFCL PR2

Mabao mawili ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Pacome Zouzoua na Aziz Andabwile yametosha kuihakikishia Yanga ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wiliete SC katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa timu hizo kutofungana Wiliete SC wakionekana kuimarika zaidi katika ulinzi tofauti na walivyocheza mechi ya kwanza nyumbani

Mabadiliko ya kipindi cha pili yaliyofanywa na kocha Romain Folz kwa kuwaingiza Edmund John na Offen Chikola nafasi ya Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya yaliiongezea Yanga kasi ya mashambulizi kupitia pembeni

Pacome alifunga bao la uongozi dakika ya 70 baada ya kupasiana na Andy Boyeli ambaye pia aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Dube

Andabwile akaweka kambani bao la pili dakika ya 86 kwa kichwa akimalizia kona ya Chikola

Yanga inasonga mbele raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-0 kufuatia ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza

Sasa itachuana na Silver Strikers ya Malawi katika mchezo wa raundi ya kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’