Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wiliete SC jana katika mchezo wa ligi ya mabingwa, kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani wanahamishia nguvu zao kwenye ligi kuu
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Mbeya ambako wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Mbeya City siku ya Jumanne, Septemba 30
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kitaondoka saa 10 jioni kuelekea Mbeya wakiwa na dhamira ya kuendeleza ubabe wao kwenye ligi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa kwanza
Baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Silver Strikers ya Malawi kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi CAFCL
Mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa Oktoba 18 huko Malawi na marudiano kupigwa Oktoba 25 uwanja wa Benjamin Mkapa