Folz afunguka maandalizi ya kuikabili Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2025
Folz afunguka maandalizi ya kuikabili Mbeya City

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Sokoine

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mkoani Mbeya mapema leo, Folz alisema ameiandaa timu yake kucheza katika mazingira yoyote

Amesema timu bora inakuwa tayari kubadilika kufuatana na mazingira, wataonyesha ubora wao katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soko mkoani Mbeya

"Ni mchezo tofauti lakini malengo yanabaki yaleyale kama zilivyokuwa mechi nyingine, tunakwenda kupambana tupate matokeo mazuri. Tunafahamu hautakuwa mchezo rahisi hivyo tutajaribu kufanya kila kitu kimbinu kuhakikisha tunafanya vizuri na tunatarajia kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wetu hapo kesho"

"Sifa ya timu yoyote bora ni kuwa na uwezo wa kucheza katika mazingira tofauti, tunatambua ugumu wa uwanja wa Sokoine na tumejiandaa kufanya vizuri, Lazima tutumie ubora wa kikosi chetu ili iwe rahisi kufanya tunachotaka, nina imani tutafanya kilicho bora," alisema Folz

Katika hatua nyingine Folz amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuwaunga mkono katika kazi wanayoifanya. Folz amesema wamekusudia kuifikisha Yanga katika sehemu ambayo haijawahi kufika, wanachohitaji ni muda na uungwaji mkono wa kila mmoja

"Tunataka kuifikisha Yanga hatua ambayo haijawahi kufika kwenye mashindano ya kimataifa, huu ni mchakato na tunaendelea kutengeneza timu taratibu. Kitu nina uhakika nacho tutafika mbali mahali ambapo hatujawahi kufika"

"Nadhani tuna kikosi bora sana na kwa sasa tunapambana kufika kwenye ubora wa juu. Ni sawa watu kutoa maoni lakini sisi kama Klabu ni lazima tuwe kitu kimoja nyakati hizi tunaposuka kitu kizuri kwa ajili ya timu yetu," alisema

Yanga ilitua Mbeya jana ambapo leo itakamilisha maandalizi yake katika uwanja wa Sokoine ambao utatumika siku ya kesho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’