Folz bado ana kibarua kingine dimba la Sokoine Novemba 1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2025
Folz bado ana kibarua kingine dimba la Sokoine Novemba 1

Baada ya kukosa ushindi dhidi ya Mbeya City juzi mchezo ukipigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Yanga itakuwa na safari nyingine ya mkoani Mbeya mapema tu mwezi Novemba pale watakapoifuata Tanzania Prisons kwa ajili ya mechi ya ligi kuu Novemba 1

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz ni wazi atapaswa kuandaa mapema mkakati wa kupata ushindi hapo Sokoine atakaporejea tena mara ya pili

Katika mchezo dhidi ya Mbeya City, Folz alieleza hali ya uwanja ilichangia vijana wake kutocheza kandanda safi na kupelekea matokeo ya suluhu

Yanga ilipocheza na Tanzania Prisons katika uwanja huo msimu uliopita, iliondoka na ushindi wa mabao 5-0 huku ikicheza kandanda la kuvutia

Wakati huo Wananchi walikuwa wakinolewa na kocha Miloud Hamdi ambaye alitimkia Misri akiinoa klabu ya Ismailia

Mwezi huu Oktoba Yanga itacheza mechi moja ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na kufungua mwezi Novemba kwa mchezo dhidi ya Prisons

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’