Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika(ACA) Eng. Hersi Said ameshiriki mkutano mkuu wa 47 wa CAF uliofanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mkutano huo umewakutanisha wawakilishi kutoka mataifa yote 54 ya Afrika kwa tukio la kihistoria lililolenga kujadili maeneo muhimu ikiwemo uongozi bora, mashindano, miundombinu na maendeleo ya pamoja kuinua na kukuza soka la Afrika.
Pichani ni Rais wa FIFA Gianni Infantino, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe na Makamu mwenyekiti wa ACA, Jessica Motaung wakiwa katika picha ya pamoja na Hersi

ADVERTISE HERE