Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi ameanza kufanya mazoezi ya timu ikiwa ni dalili njema ya kukaribia kurejea kikosini
Yao amekuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti
Uongozi wa Yanga ulilazimika kumuondoa katika orodha ya nyota waliosajiliwa akihitaji muda zaidi wa kujiimarisha
Bila shaka atakuwa tayari kurejea kikosini kwenye usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa Disemba 15
Ikumbukwe Yanga ilimsajili beki wa kati Frank Assink kwa mkopo wa miezi sita ikitarajiwa ifikapo Disemba Yao atakuwa tayari na Assink kurejea katika klabu yake ya Singida BS
ADVERTISE HERE