Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amewashukuru mashabiki wa timu hiyo nchini Malawi waliojitokeza kwa wingi kuwapokea uwanja wa ndege na kuwasindikiza hadi kwnye hotel waliyofikia
Job amesema wachezaji wanathamini kile kilichofanywa na mashabiki hao, wana deni kubwa la kuhakikisha wanawapa furaha kwa kushinda mchezo dhidi ya Silver Strikers hapo kesho
"Tunawashukuru Watanzania waliojitokeza kwa wingi kutupokea uwanja wa ndege na kutusindikiza mpaka hotelini"
"Tunajua tuna deni kubwa la kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo dhidi ya Silver Strikers hapo kesho"
"Tunajiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo, tunaamini utakuwa mchezo mgumu lakini sisi kama wachezaji ni wajibu wetu kujiandaa na kufanya vizuri katika mchezo huo," alisema Job
Yanga itakamilisha maandalizi yake leo katika uwanja wa Bingu tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu nchini Malawi
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanatarajiwa kupata sapoti kubwa ya mashabiki kwani licha ya Watanzania waishio Malawi, mabasi zaidi ya 50 yliyobeba mashabiki nayo yanatarajiwa kutua nchini humo leo