Kikosi cha Yanga kimeondoka rasmi Malawi kurejea Tanzania ambapo majira ya saa 2 usiku watatua uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Kwa mujibu wa Walter Harrison, Meneja wa Yanga, baada ya kikosi kuwasili wachezaji watapewa mapumziko hadi siku kesho Jumanne ambapo wataingia kambini Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi CAFCL dhidi ya Silver Strikers.
Yanga inahitaji ushindi wa angalau mabao 2-0 katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 25 ili kufuzu hatua ya makundi











ADVERTISE HERE