Kocha Mpya Yanga kujulikana ndani ya siku tatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Oct 2025
Kocha Mpya Yanga kujulikana ndani ya siku tatu

Licha ya kuthibitisha kuwa kocha Patrick Mabedi ataiongoza Yanga kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers, Meneja wa habari na mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mchakato wa kusaka kocha mpya unaendelea

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Kamwe alisema katika kipindi cha siku tatu zijazo Yanga inaweza kumtangaza kocha mkuu ambaye atarithi mikoba iliyoachwa na Romain Folz aliyefutwa kazi baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Silver Strikers wiki iliyopita

"Wengi mmekuwa mkiniuliza kuhusu Kocha mpya, niwaeleze tu kuwa Uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato mzuri wa kumpata kocha mpya na ndani ya siku tatu hizi mchakato huu utakuwa umekamilika"

"Kwa mantiki hiyo mchezo wetu wa tarehe 25 tutaongozwa na Care taker wetu Patrick Mabedi, na hatuna shaka kabisa na yeye kwani tunaamini kwenye uwezo wake na CV yake,” alisema Kamwe

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kamwe alisema Yanga iliingia kambini leo huku akithibitisha mshambuliaji Clement Mzize amepona majeraha na anaweza kutumika katika mchezo wa Jumamosi

"Kikosi chetu kimeingia kambini leo saa 6 mchana na kinaendelea na maandalizi ya mchezo wetu wa tarehe 25 dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, Kuhusu Clement Mzize tumeshatoa taarifa kuwa yupo fiti na kama itampendeza mwalimu basi atakuwa sehemu ya kikosi chetu tarehe 25,” alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’