Wananchi wameamua, hii ni mechi yao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
22 Oct 2025
Wananchi wameamua, hii ni mechi yao

Ukifuatilia mijadala mitandaoni tangu Yanga itangaze kuwa mashabiki wataingia bure katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers Jumamosi, utaona sauti tatu tofauti: wanaoshangilia uamuzi huo, wanaoupinga na wale wanaojifanya wachambuzi huru lakini kiukweli wana ajenda zao.

Kinachosisitizwa na wanaoupinga si hoja ya kiufundi. Hawazungumzii hamasa. Hawazungumzii nguvu ya umati. Hawataji uhalisia wa mchezo husika kwamba presha yake inahitaji nguvu ya mashabiki na sio viti vitupu. Wao wanasema ni hasara, ni matumizi ya ovyo lakini hawasemi moja kwa moja jambo walilolificha: hawapendi kuona Yanga inasonga mbele.

Mashabiki wasipoteze muda kwa kejeli

Hawa wanaoponda leo ndiyo hao hao watakaokaa viti vya mbele Jumapili kwenye vipindi vya uchambuzi redioni wakichambua na kufurahia Yanga kushindwa kufuzu makundi ya CAFCL.

Hao hawatoshi kuwa kipimo cha busara ya Yanga, maana hii ni mechi ya Wananchi, na Wananchi wameomba jambo lao: kuingia bure ili kujaza uwanja na kutoa nguvu ya kiroho, kiakili na kiushindani kwa wachezaji wao.

Yanga ni klabu ya Wanachama, wameamua

Yanga si kampuni ya mtu mmoja, ni taasisi ya wanachama. Uongozi haukubuni; umetii kilichoombwa na wamiliki halali wa klabu. Ukisikia maoni hasi ambayo hayatoki kwa wanachama wala mashabiki, elewa hapo kuna hisia za kutamani Yanga isifaulu.

Si mara ya kwanza, ni utamaduni

Hii sio mara ya kwanza Yanga kuingiza mashabiki bure uwanjani. Huu ni utamaduni wa kuheshimu mchango wa mashabiki, umeanza tangu enzi za akina Hayati Yusuf Manji, na huja tu pale panapohitajika nguvu ya pamoja kuliko hesabu ya kiingilio. Na Jumamosi ni moja kati ya hizo siku.

Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia 2–0. Mkakati wa kwanza wa ushindi ni kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mtu anayekwambia “kujazana bure si hoja” hajawahi kuona jinsi goli la tatu linaweza kupatikana dakika ya 89 kwa sababu ya vuvuzela na makelele ya watu 50,000 waliokaa upande wako.

Hii si mechi ya mijadala, ni mechi ya Wanayanga na jambo muhimu kwa Wananchi ni kwenda uwanjani kuipa sapoti timu yao halafu warudi nyumbani vifua mbele baada ya dakika 90

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
53m ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →