Job awaalika Wananchi kwa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2025
Job awaalika Wananchi kwa Mkapa

Beki na nahodha msaidizi wa Yanga SC, Dickson Job, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumamosi, Oktoba 25, 2025 katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.

Yanga ilipoteza kwa bao 1–0 kwenye mechi ya kwanza Oktoba 18, 2025 jijini Lilongwe, hivyo inahitaji ushindi wa angalau mabao 2–0 ili kutinga hatua ya makundi. Ikishinda 1–0, mshindi ataamuliwa kwa mikwaju ya penalti, na matokeo mengine yoyote yatamaliza safari ya Yanga kwenye michuano hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Job alisema kikosi hicho hakitakubali kufungwa tena nyumbani na kwamba mchezo huo ni wa kurejesha heshima na kutimiza malengo ya klabu kuingia hatua ya makundi.

“Nipo hapa kuwawakilisha wachezaji wenzangu kuwaambia tunajua mechi ni muhimu sana kushinda, tutapambana kwa jasho na damu ili tutinge hatua ya makundi,” alisema Job.

Aliongeza kuwa kufungwa ugenini hakumaanishi Yanga imefeli, bali mipango waliyoiandaa haikufanya kazi kama walivyotarajia, hivyo wameufanyia marekebisho kwa ajili ya mchezo wa kesho. Job aliwataka mashabiki kuiamini timu na kujitokeza kwa wingi uwanjani.

“Nawaomba mashabiki kesho wajue tuna jambo muhimu Mkapa, laleni mkiuwaza mchezo wa kesho, mje kwa wingi kutusapoti. Umoja wetu utatupa matunda na furaha. Mashabiki waendelee kuweka imani na sisi, kesho wataondoka kifua mbele, hatutawaangusha,” alisema.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’