Hatimaye ile siku imewadia! Jioni ya leo Jumamosi majira ya saa 11 Wananchi wanajambo lao pale uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Silver Strikers katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL)
Yanga inahitaji matokeo ya aina moja tu leo, ushindi wa tofauti ya mabao mawili utatosha kuwavusha Wananchi moja kwa moja hatua ya makundi
Silaha namba moja ya Yanga leo ni mashabiki wake, dimba la Benjamin Mkapa linapaswa kuwa 'full' na kuhakikisha mashabiki wanashangilia muda wote ili kuwaweka wapinzani wao katika presha kubwa
Yanga tayari imetangaza utaratibu wa kuingia dimba la Mkapa ambapo mageti yatafunguliwa kuanzia saa 4 asubuhi na kufungwa saa nane mchana
Hivyo mashabiki watakuwa na saa 4 tu kujaza dimba la Mkapa. Hatua hizi zimechukuliwa ili kuepuka matukio ya vurugu ambayo yanaweza kujitokeza kama mageti hayatafungwa mapema
Kaimu kocha mkuu wa Yanga Patrick Mabedi amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa kikosi chake kiko tayari na leo watarajie kuona sura na tabia tofauti ya timu yao
Leo tutashuhudia 'ukatili' wa aina yake kutoka kwa wachezaji wa Yanga mbele ya lango la Silver Srikers
Kila la kheri Yanga, kila la kheri mabingwa wa nchi....