Yanga imetinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Silver Strikers katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Dickson Job na Pacome Zouzoua yalitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo katika mchezo ambao pengine Wananchi walistahili kuondoka na ushindi mnono zaidi
Yanga ilitawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza, vijana wa kocha Patrick Mabedi wakionekana kuwa na ari na morali ya kusaka ushindi mapema
Unaweza kusema haikuwa siku nzuri kwa Prince Dube ambaye nafasi kadhaa za wazi zilipotelea mguuni mwake
Yanga inafuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 katika mechi zote mbili
Pongezi kwa mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza kwa wingi kujaza dimba la Mkapa na zaidi leo walishangilia muda wote
Yanga hiyooooooo makundi...!