Baada ya kumtambulisha kocha mkuu Pedro Goncalves kutoka Ureno, Yanga pia imemuajiri kocha msaidizi Filipe Pedro naye kutoka Ureno.
Makocha hao wamefanya kazi pamoja katika klabu mbalimbali na haishangazi wakiungana tena kwenye majukumu makubwa ya kuinoa Yanga
Majukumu yao ya mwisho pamoja ilikuwa wakiinoa timu ya Taifa ya Ureno. Pedro pia amewahi kuzinoa Ekenas ya Finland, Casa ya Ureno na timu za vijana za Sporting Lisbon

Karibu Jangwani Pedro...!
ADVERTISE HERE