Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Silver Strikers sio tu umeipeleka Yanga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, lakini pia ile bonasi ya goli la Mama imehusika.
Baada ya mchezo Yanga ikakunja kitita cha Tsh Milioni 20, fedha za bonas ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. Samia Suluhu Hassan.
Bonasi hiyo ikakabidhiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa
Yanga imekusanya jumla ya Tsh Milioni 35 katika mechi za mtoano ikishinda jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Wiliete Sc na pia kushinda mabao 2-1 katika mchezo dhidi ya Silver Strikers




ADVERTISE HERE