Yanga kuendeleza ubabe dhidi ya Mtibwa Sugar leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2025
Yanga kuendeleza ubabe dhidi ya Mtibwa Sugar leo?

Burudani inarejea kwa Wananchi uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar, wakati mabingwa wa nchi Yanga wakiwakabili Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Baada ya kucheza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya Pamba Jiji katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga imerejea tena KMC Complex, dimba la Mkapa likisitishwa matumizi kwa mechi za ndani.

Yanga ina historia ya kibabe hapo KMC Complex hivyo urejeo wao umepokelewa kwa furaha na mashabiki.

Msimu uliopita baada ya kupoteza mechi mbili katika dimba la Azam Complex, Yanga ikahamia KMC Complex ambapo walishinda mechi zote walizocheza katika uwanja huo

Yanga inaingia uwanjani leo ikiwa tayari imecheza mechi mbili za ligi msimu huu na kukusanya pointi nne kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji na matokeo ya 0-0 dhidi ya Mbeya City.

Rekodi zinaonyesha katika mechi kumi za Ligi Kuu zilizopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Yanga imeshinda tisa na sare moja. Mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ilikuwa Aprili 17, 2019. Katika ushindi wa mechi hizo tisa, nane ni mfululizo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’