Yanga imetakata uwanja wa KMC Complex ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Mabao ya mashuti ya mbali yaliyofungwa katika kila kipindi na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' na Ecua Celestin yalitosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu
Haikuwa mechi nyepesi Mtibwa Sugar wakicheza kwa nidhamu katika safu ya ulinzi wakiwanyima washambuliaji wa Yanga nafasi ndani ya eneo la hatari na hivyo mara kadhaa kulazimika kupiga mashuti ya mbali
Ilikuwa mechi ya kwanza kwa kocha Pedro Goncaves ambaye ndio kwanza ameanza majukumu ya kuwanoa Wananchi
Goncalves leo amepata nafasi ya kusimama katika benchi na bila shaka ameona nini anapaswa kufanya ili kuboresha hasa eneo la safu ya ushambuliaji





ADVERTISE HERE