Baada ya Bodi ya ligi kutangaza rasmi kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC Novemba 08, kikosi cha Yanga hakikuwa na muda wa kupoteza kwani jana kilirejea mazoezini kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya KMC.
Jumapili Novemba 09 Yanga itakuwa mwenyeji wa kMC katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves aliongoza mazoezi hayo yaliyofanyika katika viunga vya Avic Town, Kigamboni.
Aidha maandalizi hayo pia ni mechi za hakua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) ambapo mwishoni mwa mwezi huu mechi mbili zitapigwa.
Yanga itaanza nyumbani dhidi ya AS FAR na kisha kusafiri Algeria kuikabili JS Kabylie ya nchini humo.
ADVERTISE HERE