Ijumaa ya Novemba 14, timu ta Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa uwanja wa Al Salam, jijini Cairo ikicheza mechi ya kirafiki na Kuwait.
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha Stars ambacho kitaingia kambini chini ya kaimu kocha mkuu Miguel Gamondi kujiandaa na mchezo huo.
Nyota watano wa Yanga nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mohamed Hussein na Mudathir Yahya wamejumuishwa katika kikosi hicho.

ADVERTISE HERE