Yanga imepanda kileleni mwa msimamo wa ligi ikiichapa KMC mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Mabingwa hao watetezi walitua vyema dakika 45 za kipindi cha pili baada ya kubanwa mbavu na kulzimishwa sare ya bao 1-1 kwenye dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Alikuwa ni Maxi Nzengeli aliyeitanguliza Yanga mapema akimalizia pasi ya Pacome Zouzoua lakini KMC wakarejea mchezoni dakika chache baadae kupitia kwa Daruweshi Saliboko aliyemalizia mpira uliotemwa na Djigui Diarra.
Mabadiliko yaliyofanywa na mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves kwenye kipindi cha pili akiwaingiza Andy Boyeli, Celestin Ecua na Shekhan Khamis yaliinufaisha Yanga ikifanikiwa kuongeza mabao mengine matatu kupitia kwa Pacome huku Boyeli akipachika mabao mawili.
Ecua na Boyeli waliivuruga safu ya ulinzi ya KMC wawili hao wakishirikiana katika mabao yote mawili.
Ni ushindi muhimu kwa Yanga unaowapeleka juu ya msimamo kwa mara ya kwanza msimu huu.




