Jumamosi ya Novemba 22 mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga watakuwa nyumbani kuanza kampeni ya kuisaka robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya AS FAR ya Morocco.
Ratiba ya mchezo huo imethibitishwa ambapo utapigwa Jumamosi Novemba 22 katika uwanja wa New Amaan Complex, saa 11 jioni.
Itakuwa mara ya kwanza Yanga kutumia dimba la Amaan katika mechi za makundi ya ligi ya mabingwa.
Msimu uliopita Yanga ilicheza mechi ya mkondo wa pili hatua ya awali dhidi ya CBA ya Ethiopia na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0
Yanga ina rekodi ya aina yake katika uwanja huo kwani tangu ulipofanyiwa maboresho, wananchi hawajawahi kupotezo mchezo.
Ni zama mpya kwa Yanga kucheza mechi zake za Kimataifa katika dimba la Amaan.
ADVERTISE HERE