Yanga yajipanga kumrejesha Behlulovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Nov 2025
Yanga yajipanga kumrejesha Behlulovic

Uongozi wa Yanga huenda ukamrejesha aliyekuwa kocha wa viungo wa timu hiyo Adnan Behlulovic aliyehudumu kwenye nafasi hiyo wakati Yanga ikinolewa na Sead Ramovic.

Baada ya maoni na mapendekezo ya Wanayanga wengi juu ya kutoridhishwa na utimamu wa wachezaji wao, ni kama uongozi umesikia kilio na sasa wako mbioni kumshusha Behlulovic kuchukua nafasi ya Mokaila Tsephang ambaye alirejea Botswana baada ya kupata msiba wa kufiwa na mama yake mzazi.

Baada ya Yanga kusitisha mkataba wa kocha Romain Folz na wasaidizi wake, ni Mokaila pekee aliyekuwa amesalia benchini yakiwa ni mapendekezo ya kocha mpya Pedro Goncalves aliyehitaji kufanya nae kazi kwa muda ili kujiridhisha kama anatosha au la.

Wakati Yanga inanolewa na Ramovic, 'Gusa Achia Twende Kwao' ilizaliwa, soka la kasi huku wachezaji wakifanya 'pressing' bila kuchoka. 

Behlulovic ndiye aliyehakikisha wachezaji wanakuwa fit na 'natanki' yao yamejaa muda wote wa mchezo.

Mashabiki bado wana taswira ya Yanga hiyo na pengine ndio sababu licha ya timu yao kuendelea kufanya vyema kwenye ligi, bado wanaona kuna kitu kinakosekana.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’