Yanga Soccer School yazinduliwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2025
Yanga Soccer School yazinduliwa

Klabu ya Yanga leo imezindua rasmi mradi wa Yanga Soccer School katika viwanja vya Speedsports–Muhimbili, hatua inayolenga kuibua na kuendeleza vipaji vya soka nchini.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, kocha mashuhuri barani Afrika, Dkt. Pitso Mosimane, kutoka Afrika Kusini ameleza furaha yake kushiriki uzinduzi huo akiwa mmoja wa waliomshauri Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kuanzisha shule hiyo.

Mosimane amesema licha ya taifa lake kuwa na dabi kubwa kati ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, tukio alilolishuhudia katika Kilele cha Wiki ya Mwananchi lilikuwa la kipekee, na idadi ya mashabiki wa Yanga ilimshawishi kupendekeza uanzishwaji wa mradi huo.

"Namshukuru sana Rais wa Yanga SC, Mimi na Injinia ni marafiki wa muda mrefu sana. Niliwahi kuja hapa kwa ajili ya Mwananchi Day. Ama kwa hakika ni siku pekee na ya kufana sana. Mashabiki wa Yanga wanaipenda sana timu yao. Hongereni sana. Nyie ni mfano wa kuigwa"

"Siku ya mwananchi nilivutiwa sana na mwamko wa mashabiki. Tukiwa kwenye gari nikamwambia Rais wa Yanga anzisha Shule ya Soka. Nimefurahi sana hatimaye leo nipo kwenye uzinduzi. Namshukuru pia rafiki yangu Arafat Haji, amenipokea vizuri. Yanga ni familia yangu kwa muda mrefu,” alisema Mosimane

Akiazungumza katika uzinduzi huo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisema Yanga Soccer Family imeanzishwa kwa ajili ya kuwaandaa vijana na kuwapa maarifa ya mpira wa miguu ambayo yatawaweka tayari kupiga hatua kubwa zaidi.

“Yanga Soccer Family ni jukwaa ambalo linaleta watu wataaluma tofauti tofauti, vijana wanaotengenezwa hapa wataondoka wakiwa na maarifa ya kutosha. Tunatengeneza vijana wa kesho ambao wanapenda mpira lakini wanaujua vyema na jamii ya kesho itakwenda kuupenda mpira na kuushabikia"

"Niwapongeze sana wazazi ambao wametuamini na kuleta vijana wao kuwasijili kwenye Yanga Soccer Family. Jukwaa hili ni jukwaa muhimu sana kwa ukuaji wa soka la kizazi cha kesho. Hawa watoto watakwenda kuwa msaada mkubwa kwa familia yao na kwa taifa kiujumla kupitia soka"

"Mradi huu ni mradi endelevu ambao tutachukua watoto wa U-11, U-13 na U-15. Hatutaishia mkoa wa Dar Es Salaam pekee yake bali tutatanua wigo kwa maeneo mbalimbali Tanzania. Jukwaa hili litatusaidia sana kwenye kuinua vipaji ambavyo tunaweza kuvitumia kwenye timu zetu za vijana"

“Tumeongea na Kocha Pitso Mosimane ambaye amekubaki ombi letu la kutoa mafunzo kwa makocha wetu wa vijana. Lengo letu ni kutumia falsafa ya timu yake ya soka na kuimarisha falsafa yetu pia hapa. Tunamshukuru sana Kocha Mosimane kwa kukubali wito wa kujiunga nasi siku hii ya historia,” alisema. Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’