Ikiwa imesalia wiki moja kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya AS FAR, Wananchi wanaendelea na maandalizi yao KMC Complex kujiandaa na mchezo huo.
Imeelezwa kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ametaka kikosi chake kiwahi visiwani Zanzibar ili wapate muda wa kutosha kuzoea mazingira.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imedokeza kuwa huenda mabingwa hao wa Tanzania Bara wakaelekea Zanzibar siku ya Jumatatu, ampapo watakuwa na takribani siku tano za kujifua visiwani humo.
Yanga imeweka malengo ya kuanza vyema hatua ya makundi kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.
Wananchi wako kundi D linaloaminika ndio kundi gumu zaidi likiundwa timu nyingine kama Al Ahly, AS FAR na JS Kabylie.
Unaweza kusema ni Yanga dhidi ya timu kutoka Afrika ya Kaskazini, timu mbili pekee zikiwa na nafasi ya kufuzu robo fainali