Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa mlinzi wa kushoto wa Yanga Chadrack Boka.
Akiwa katika msimu wake wa pili na Wananchi, Boka ameendelea kudhihirisha kwa nini Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alifunga safari kumfuata DR Congo alikokuwa anaitumikia Fc Lupopo kukamilisha usajili wake.
Msimu wake wa kwanza ulikumbwa na majeraha ya mara kwa mara lakini msimu huu ameanza vyema licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' aliyetua kwa Wananchi katika dirisha lililopita akitokea klabu ya Simba.
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake..

HAPPY BIRTHDAY BOKA...
ADVERTISE HERE